MWANANYAMALA RRH YAWAFIKIA WATU 150 SIKU YA KWANZA YA MAADHIMISHO YA WIKI YA AFYA YA AKILI.

Posted on: October 4th, 2023


Katika kuadhimisha wiki ya Afya ya akili Duniani, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala imeandaa maadhimisho hayo kwa kutoa elimu na uchunguzi wa afya ya akili, uchangiaji  damu, vipimo vya magonjwa ya ndani kama kisukari, shinikizo la damu, uchunguzi ya saratani ya shingo ya uzazi, upimaji wa Virusi  vya UKIMWI, Homa ya Ini na Uzito.

Aidha katika siku ya kwanza ya maadhimisho haya, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala imekusanya uniti 28 za damu pia imeweza kufikia watu 150  waliojitokeza kupata huduma hizo ambazo zinatolewa bila malipo lengo likiwa ni kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuweza kutatua changamoto zao kwa wakati.

Huduma za elimu na uchunguzi wa afya ya akili, vipimo vya magonjwa ya ndani na zoezi la uchangiaji damu zitaendelea hadi oktoa 8, 2023 kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.