Saratani Ya Shingo ya kizazi

Posted on: February 23rd, 2020

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Ni nini chanzo chake

Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na aina ya kirusi kinachoitwa Human Papilloma (HPV). Kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukuzi ya HPV


Dalili zake

 • Kutokwa na majimaji au uchafu kusiko kwa kawaida ukeni  Kutokwa na damu kidogo au nyingi ukeni wakati wa kujamiiana 
 • Kutokwa na damu kidogo au nyingi ukeni wakati ambao mwanamke hayuko kwenye hedhi. 
 • Maumivu wakati wa kujamiiana 
 • Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake waliokwisha koma hedhi  Maumivu sehemu ya nyonga au chini ya tumbo


Tabia hatarishi zinazochangia saratani ya shingo ya kizazi

 • Kuanza ngono mapema katika umri mdogo (chini ya miaka 18) 
 • Uvutaji wa sigara au tumbaku 
 • Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi 
 • Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi hasa yale yatokanayo na wanyama 
 • Kutokula mboga za majani na matunda mara kwa mara 
 • Kuzaa idadi kubwa ya watoto hasa wanawake walioanza kuzaa wakiwa na umri mdogo (chini ya miaka 18)


Uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi?

Kwa kufanyiwa uchunguzi wa shingo ya kizazi na wataalamu wa afya angalau mara 1 kwa mwaka


Kuepuka uwezekano wa kupata saratani ya shingo ya kizazi

 • Kuepuka ngono katika umri mdogo, chini ya miaka 18 
 • Kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu  Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana 
 • Kuepuka uvutaji wa sigara na tumbaku  Kula matunda na mboga za majani kwa wingi 
 • Kuepuka matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula hasa yale yatokanayo na wanyama 
 • Kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi angalau mara 1 kwa mwaka 
 • Kuwahi mapema kwa uchunguzi na matibabu punde tu upatapo dalili