Magonjwa ya Moyo

Posted on: February 23rd, 2020

Magonjwa ya moyo

Moja wapo ya sababu za magonjwa ya moyo ni kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye misuli ya moyo. Kuziba kunaweza kusababishwa na mafuta yanayotokana na chakula kinacholiwa. Mafuta haya huganda katika kuta za mishipa hiyo, hali ambayo hutokea pole pole na huchukua muda mrefu hadi mishipa kuziba kabisa. Shinikizo la damu, tumbaku, uzito uliozidi na kutofanya mazoezi huchangia sana uharibuvu huu.

 • Dalili za magonjwa ya moyo

Kadiri mishipa ilivyoziba, misuli ya moyo hukosa oksijeni na virutubishi hali ambayo inasababisha dalili zifuatazo:

 • Maumivu ya kifua ambayo hutokea zaidi mtu anapojitahidi kujishughulisha na kutoweka anapopumzika
 • Moyo kwenda haraka 
 • Uchovu na kukosa nguvu ya kufanya kazi 
 • Ikiwa sehemu kubwa ya moyo imeathirika, moyo hushindwa kabisa kufanya kazi.Kuzuia magonjwa ya moyo

 • Hakikisha uzitowako uko katika kiwangokinachofaa kwa kufuata ulaji na mtindo bora wa maisha 
 • Chagua vyakula vyenye mafuta kidogo kama vile matunda, mbogamboga, nafaka zisizokobolewa. 
 • Chagua nyama na maziwa yasiyo na mafuta mengi. 
 • Epuka vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta mengi kama siagi, keki, chokoleti; na vyakula vilivyokaangwa kama chipsi, kuku, na maandazi, sambusa na vitumbua
 • Lehemu ni aina maalum ya mafuta ambayo mara nyingi hupatikana katika maini, sehemu ya njano ya yai, siagi, barafu, na nyama yenye mafuta mengi. Aina hii ya mafuta huongeza sana uwezekano wa kuziba mishipa ya damu hivyo epuka kula vyakula hivi vyenye lehemu nyingi. 
 • Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili kwa dakika 30 hadi 60 kila siku.  Epuka kukaa bila kufanya shughuli yoyote. 
 • Epuka uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku ambavyo huchangia katika kuleta magonjwa ya moyo 
 • Epuka unywaji wa pombe kwani unachangia kwenye kuongeza uzito na huingilia matumizi mazuri ya chakula mwilini

Aina za magonjwa ya moyo

Matibabu ya magonjwa ya moyo

Kiharusi