Kisukari

Posted on: February 23rd, 2020

Kisukari

Ugonjwa wa kisukari ni hali aambayo inatokea wakati sukari katika damu inakuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu. Ili mwili uweze kutumia sukari iliyotoka kwenye vyakula huhitaji kichocheo cha insulini. Insulin husaidia sukari kuingia kwenye chembechembe hai ili kutengeneza nishati-lishe.

Aina za kisukari 

Kuna aina mbili kuu za kisukari ambazo ni;

 1. Kisukari kinachotegemea insulini
 2. Kisukari kisichotegemea insulini

Kisukari kinachotegemea insulini

Kisukari kinachotegemea insulin au “type one diabetes” husababishwa na upungufu au ukosefu wa kichocheo kinachotengenezwa kwenye kongosho kinachoitwa insulini.

Aina hii ya kisukari hudhibitiwa kwa kutumia sindano ya insulin kwani mwili huwa unashindwa kutengeneza kichocheo hiki, pamoja na kurekebisha ulaji. Mala nyingi aina hii ya kisukari huwapata watu wenye umri mdogo (watoto na vijana). Villevile mtu hawezi kurithi iwapo kuna historia ya kisukari katika familia.

Kisukari kisichotegemea insulin

Kisukari kisichotegemea insulin au “type two diabetes” husababishwa na mwili kushindwa kutumia sukari. Mwili wa mtu mwenye aina hii ya sukari huweza kutengeneza insulini ya kutosha lakini haitumiki kuuweesha mwili kutumia sukari na hivyo sukari katika damu huwa katika kiwango cha juu

Aina hii ya kisukari huweza kudhibitiwa kwa kutumia vidonge pamoja na kurekebisha ulaji; au kwa kurekebisha ulaji pekee. Mara nyingi huwapata watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 40 na kuendelea

Kumbuka

 • Ufanisi wa tiba ya aina zote za kisukari hutegemea sana ulaji unaozingatia masharti yatolewayo na mtoa huduma za afya
 • Muonekano wa mgonjwa wa kisukari kinachotegemea insulin mara nyingi huwa ni mwembamba wakati Yule mwenye kisukari kisichotegemea insulin huwa mnene.

 

Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata kisukari

 • Uzito uliozidi (overweight) au unene uliokithiri (obesity)
 • Kutofanya mazoezi
 • Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi
 • Kuwa na shinikizo kubwa la damu
 • Matumizi ya sigara na bidhaa nyingine za tumbaku
 • Kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40
 • Historia ya kuwa na kisukari katika familia

Dalili za ugonjwa wa kisukari

 • Kukojoa mara kwa mara
 • Kusikia kiu sana
 • Kusikia njaa sana
 • Kuchoka sana na kukosa nguvu bila kufanya kazi
 • Kutoona sawa sawa
 • Kupungua uzito bila kukusudia
 • Kusikia kizunguzungu
 • Kuwa na maambukizi ya ngozi nz vidonda visivyopona upesi
 • Baadhi ya viungo vya mwili kama vidole vya miguu na mikono kufa ganzi

Madhara ya kisukari

Ugonjwa wa kiskari usipodhibitiwa huleta madhara mbalimbali mwilini. Madhara haya huwa makubwa zaidi hasa pale mgonjwa anapokua hazingatii masharti ya matibabu na ulaji bora.

Kuna madhara ya muda mfupi na muda mrefu

Kushuka kwa kiwango cha sukari katika damu

Hali hii hutokea pale ambapo sukari hushuka kuliko kawaida. Hii inaweza kutokana na kutumia dawa kuzidi kipimo, kunywa pombe, kufanya mazoezi bila kula na kutokula kwa muda mrefu.

Dalili za kushuka kwa kiwango cha sukari katika damu

 • Moyo kwenda mbio
 • Mwili kutetemeka
 • Kusikia njaa
 • Kusikia kizunguzungu
 • Kuona mbali (double vision)
 • Kuchanganyikiwa
 • Kutokwa jasho kwa wingi
 • Kuchoka sana

Hali hii ikizidi mgonjwa huweza kupoteza fahamu na hatimaye kupoteza maisha kama hatapata matibabu mapema.

Kama mgonjwa akipatwa na hali hii asipewe kitu chenye sukari, ikiwemo glukosi, soda au juisi.


Kumbuka

 

 • Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe kinywaji au chakula
 • Anaweza kuwekewa glukosi kidogo kati ya shavu na fizi
 • Awahishwe katika kituo cha huduma za afya haraka iwezekanavyo

 


 

Kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu

Hali hii hutokea pale kiwango cha sukari kinapokuwa juu kuliko kawaida. Hii inaweza kutokea wakati mgonjwa anapoacha kutumia dawa, asipotunza dawa vizuri, asipotumia dawa kwa usahihi, anapoacha kufuata masharti ya ulaji unaotakiwa, anapopata maabukizo au maradhi mfano malaria, flu, nimonia nk


Dalili za kupanda kiwango cha sukari katika damu

Kupumua haraka haraka

Kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa usiku

Kua na kiu au kukauka koo

Kunywa maji mengi

Kutoona vizur (ukungu)

Kuchoka bila sababu

Miguu na mikono kuchoma

Kizunguzungu

Kuongezeka mapigo ya moyo au moyo kwenda mbio

Kuchanganyikiwa

Kupungukiwa na maji mwilini

Kupoteza fahamu na hatimaye kupoteza maisha kama mgonjwa hatapata matibabu mapema

Kumbuka

Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe chochote bali awahishwe katika kituo cha kutoa huduma za afya haraka sana                                                                                                                                                 

Madhara ya muda mrefu 

 • Upofu
 • Maradhi ya figo
 • Maradhi ya moyo
 • Vidonda kutopona upesi na hatari ya kukatwa mguu
 • Kufa ganzi na kupoteza hisia za mikono na miguu
 • Kiharusi

Kuzuia kisukari

 • Kula mlo kamili angalau mara tatu kwa siku
 • Epuka kula chakula kingi kupita kiasi
 • Epuka kula chakula chenye mafuta mengi au sukari nyingi
 • Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara
 • Pima sukarikatika damu mara kwa mara, angalau mara moja kwa mwaka
 • Epuka matumizi ya pombe za aina zote
 • Epuka matumizi ya sigara , bidhaa nyingine za tumbaku na madawa ya kulevya.

Jinsi ya kuishi na kisukari

Dhibiti ulaji wako

 • Kula mlo kamili uliotayarishwa kutokana na angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la vyakula
 • Kula vyakula vya nafaka kama ulezi, mtama, uwele, ma nafaka zisizokoboewa kwa mfano dona, ngano, au shairi
 • Kula mboga mboga kwa wingi kwa mfano mchicha, matembele, karoti, majani ya maboga, kisamvu, mlenda nk
 • Kula kiasi kidogo cha vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi katika mlo
 • Kula vyakula vya jamii ya kunde kama mboga (sehemu ya mlo) kwa mfano maharagwe, njegere, mbaazi, kunde, choroko, nk
 • Kula matunda kwa kiasi mfano ndizi au chungwa moja au kipande cha papai au embe kubwa katika kila mlo
 • Kunywa maji kwa wingi
 • Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi kama jamu, asali, chokoleti, pipi, bazooka, aiskrimu, na juisi bandia
 • Epuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi
 • Epuka unywaji wa pombe

Fanya mazoezi mara angalau nusu saa kwa siku

Tunza miguu yako kwa makini

 • Epuka kuvaa viatu au soksi zinazo bana
 • Epuka kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu ambacho huweza kusababisha kuanguka na kuumia
 • Osha miguu yako kwa maji safi na kausha vizuri hususan katikati ya vidole
 • Usitembee bila kuvaa viatu
 • Vaa viatu vya wazi na vyenye kisigino kifupi
 • Epuka kijiumiza, na unapokua na kidondatibu mapema

Epuka msongo wa mawazo zingatia

 • Afya ya kinywa kwa kupiga mswakiangalau mara mbili kwa siku
 • Usafi wa mwili
 • Taarifa a elimu kuhusu kisukari
 • Taarifa na elimu kuhusu kisukari
 • Masharti ya dawa na ulaji
 • Kuhudhulia kliniki kama inavyoshauriwa
 • Kumuona daktari mapema mara unapopata tatizo lolote la kiafya


Angalizo

 • Awe makini na ulaji wake, hussani akiwa shuleni
 • Azingatie na aoanishe muda wa kupata sindano ya insulin na muda wa kula
 • Asaidiwe kuepuka kula vyakula visivyo bora kilishe
 • Afikiriwe na aangaliwe wakati wa michezo, mazoezi, na kazi za kutumia nguvu
 • Waalimu washirikiane n wazazi au walezi kuhakikisha motto anapata asusa zenye virutubishi muhimu anapokua shuleni