MWANANYAMALA RRH YAUNGANA NA TAASISI ZINGINE ZA AFYA KUADHIMISHA WIKI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KITAIFA

Posted on: November 13th, 2023

MWANANYAMALA RRH YAUNGANA NA TAASISI ZINGINE ZA AFYA KUADHIMISHA WIKI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KITAIFA

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala inashiriki maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza Kitaifa yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala inashiriki maadhimisho hayo kwa kutoa wataalamu kutoka kada mbalimbali wanaoshirikiana na wataalamu kutoka taasisi nyingine za afya kutoa huduma za kimatibabu na ushauri wa kiafya, zinazotolewa bure katika viwanja hivyo.

Wataalamu hawa wanashiriki katika kutoa huduma za upimaji wa Kisukari, Homa ya Ini, uchunguzi wa afya ya akili, huduma za kifamasia, elimu ya lishe, uchunguzi wa macho pamoja na uchunguzi wa Kinywa na meno.

Maadhimisho hayo yaliyoanza rasmi tarehe 11 Novemba, yatahitimishwa tarehe 18 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa (Mb).