HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MWANANYAMALA YASHIKWA MKONO

Posted on: September 7th, 2023


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dr, Zavery Benela leo amepokea vifaa tiba kutoka Taasisi ya Bima ya Taifa ikiwa ni sehemu ya shughuli za kurudisha kwa jamii za Taasisi hiyo.

Mbali na utoaji wa Vifaa tiba, Taasisi ya Bima ya Taifa imetoa kadi za Bima ya jamii kwa watu 50 wenye mahitaji maalum na wenye matibabu ya muda mrefu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala. 

Akiwasilisha salamu, Dr. Benela ameishukuru Taasisi ya Bima ya Taifa kwa kuichagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala katika kuwagusa wagonjwa hao wenye uhitaji kwa kuwapatia bima za afya na kwa kupatiwa vifaa tiba hivyo ambavyo vitatumika katika kutoa huduma za matibabu hasa ya uzazi. 

Nae, Mwenyekiti wa Taasisi ya Bima Tanzania Bi. Magreth Mwaikongo ameshukuru uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwa kuwatambua wenye uhitaji na kuruhusu wapatiwe Bima hizo za afya watakazotumia kupata matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja.