Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwa kushirikiana na Taasisi JAI Tanzania leo imeadhimisha kilele cha wiki ya Wiki ya JAI Kitaifa
Posted on: August 13th, 2023
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwa kushirikiana na Taasisi JAI Tanzania leo imeadhimisha kilele cha wiki ya Wiki ya JAI Kitaifa, maadhimisho yaliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala na kuambatana na zoezi la uchangiaji damu ambapo jumla ya chupa za damu 67 zimekusanywa.
Akiwasilisha salamu za Serikali, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mussa Azan Zungu amehimiza wananchi kujijengea utaratibu na mazoea ya kula vyakula vinavyojenga afya na kuchangia kuongeza damu mwilini.
Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Dkt. Zavery Benela ameishukuru Taasisi ya JAI Tanzania kwa kuifanya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kuwa sehemu ya Kilele cha maadhimisho, kujitolea kuhamasisha na kuchangia damu kwa wingi.
"Katika matibabu yetu, damu haiuzwi, naomba niwahakikishie damu hii mnayochangia hapa tunahikisha inafikia walengwa bure kama ninyi mnavyochangia bure na kwa hiari". Amesema Dkt. Benela.
Zoezi la Uchangiaji damu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala ni endelevu hivyo wananchi wote mnakaribishwa kufika kuchangia damu kwa hiari kila siku kuanzia saa 1;30 asubuhi.
Changia Damu, Okoa Maisha. @changiadamutz @wizara_afyatz