Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala ikiendesha Mafunzo ya Uchangiaji Damu kwa Maafisa JWTZ

Posted on: August 31st, 2023


Katibu wa Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Ndg. Rajabu Omari, Leo amewapongeza na kuwashukuru Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuchangia damu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala. 

 Zoezi hilo la uchangiaji damu ni sehemu ya  maadhimisho ya miaka 59 ya Jeshi hilo ambapo uniti 19 za damu zimekusanywa.

Ndg. Rajabu Omari ametoa wito kwa wananchi na Taasisi nyingine kuiga mfano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuendelea kuchangia na  kuhamasisha uchangiaji damu katika vituo rasmi vya uchangiaji damu nchini.